Safari ya Ufini

Maandalizi ya Safari ya Ndege

Safari ya Ufini ni kwa usafiri wa ndege. Safari huanza kwenye Uwanja wa ndege. Kwa sababu kila abiria anaruhusiwa ...

Kuingia

Unapokuwa ukielekea uwanja wa ndege ni muhimu kuwahi mapema, mambo mengi hufanyika kabla ya kuabiri ...

Kutembea Ndani ya Uwanja wa Ndege

Unapotembea ndani ya uwanja wa ndege kutoka ghorofa moja hadi nyingine unaweza kutumia kambarau, ngazi ya ...

Ukaguzi wa Pasi

Kisha utaenda sehemu ya kukagua pasi. Utawasilisha hati zako za kusafiri na tikiti ya ndege ili pasi yako ikaguliwe. Karani ...

Ukaguzi wa Usalama

Kisha unaenda kufanyiwa ukaguzi wa usalama. Unapoenda kufanyiwa ukaguzi wa usalama, kila mtu ahakikishe ...

Kuabiri Ndege

Baada ya ukaguzi utaingia eneo la safari za kimataifa na uende kwenye lango ambalo ndege yako itapaa ikiwa. Utaambiwa ...

Kuwasili Ufini

Kuwasili nchini Ufini, Helsinki, kwenye uwanja wa ndege. Kwanza utaonyesha hati zako za kusafiri katika sehemu ya kukagua ...




Maandalizi ya Safari ya Ndege

Safari ya Ufini ni kwa usafiri wa ndege. Safari huanza kwenye Uwanja wa ndege. Kwa sababu kila abiria anaruhusiwa kusafiri na mzigo wa kilo 20, hakikisha unapanga vitu ambavyo utasafiri navyo na vitu utakavyoacha kabla ya safari. Ingawa katika safari za ndege za kimataifa mzigo wa zaidi ya kilo 20 unaruhusiwa, katika safari za ndani ya Ufini, huwezi kubeba mzigo zaidi ya kilo 20.

Hakikisha unabeba hati zako za kusafiri na tikiti za ndege unapokuwa ukisafiri. Ni muhimu kuchukua vyeti vyako vya elimu. Huna haja ua kubeba vyombo vya jikoni au bidhaa nyingine za nyumbani. Chakula na vinywaji haviruhusiwi kupita sehemu ya usalama.

Kuingia

Unapokuwa ukielekea uwanja wa ndege ni muhimu kuwahi mapema, mambo mengi hufanyika kabla ya kuabiri ndege. Uwanja wa ndege ni mkubwa na kuna watu wengi. Ni vizuri kuwashika mikono watoto wadogo na kukaa karibu, ili yeyote asipotee katika umati. Kuna vigari katika uwanja wa ndege vya kutumia kuweka mzigo wako. Unaweza kuenda kwa kigari hicho hadi sehemu ya abiria kusubiria kabla ya safari.

Katika sehemu ya kuingia wasilisha hati zako za kusafiria na tikiti za ndege. Baada ya kuwasilisha hati karani atakuomba uweke mzigo wako kwenye mkanda na wataupima. Unaweza kubeba mkoba mdogo kwenye sehemu ya abiria kusubiria ndege, lakini mizigo mingine huenda sehemu ya mizigo ndani ya ndege kiotomatiki. Vitu viowevu, vyenye makali haviruhusiwi ndani ya mkoba unaoingia nao kwenye ndege. Utapewa risiti ya mzigo utakaowekwa kwenye ndege na hakikisha unatunza risiti hiyo. Risiti hiyo ni uthibitisho muhimu iwapo mzigo utapotea wakati wa safari. Mzigo unaweza kutafutwa baadaye kwa kutumia risiti hiyo.

Karani atakurudishia hati za kusafiri, tikiti za ndege na risiti ya mzigo. Iwapo unabadilisha ndege katika safari yako, bila shaka utapewa tikiti ya ndege ya kufaulisha. Kwenye tikiti hiyo kuna taarifa kuhusu lango la kuondoka na nambari ya kiti chako kwenye ndege. Kabla ya kuabiri ndege utaonyesha tikiti hiyo mara kadhaa.

Kutembea Ndani ya Uwanja wa Ndege

Unapotembea ndani ya uwanja wa ndege kutoka ghorofa moja hadi nyingine unaweza kutumia kambarau, ngazi ya umeme au ngazi ya kawaida. Kwa sababu ngazi ya umeme hukimbia kiotomatiki ni muhimu kuangalia pembe za sketi au visigino vya viatu visinase baina ya ngazi. Huruhusiwi kupanda ngazi ya umeme ukiwa na kigari. Unapotumia kigari kubebea mzigo lazima utumie kambarau. Pia unaweza kuingia kwenye uwanja wa ndege kama unatumia kiti cha magurudumu. Katika hali kama hii unapaswa kuwa na mtu wa kukusaidia.


Ukaguzi wa Pasi

Kisha utaenda sehemu ya kukagua pasi. Utawasilisha hati zako za kusafiri na tikiti ya ndege ili pasi yako ikaguliwe. Karani atachukua hati za kusafiri na azipige muhuri. Kila mtu huenda mwenyewe kwenye dirisha la kukagua pasi. Familia inaweza kwenda pamoja na watoto wadogo.

Ukaguzi wa Usalama

Kisha unaenda kufanyiwa ukaguzi wa usalama. Unapoenda kufanyiwa ukaguzi wa usalama, kila mtu ahakikishe hajabeba chakula chochote, vitu viowevu, mkasi, visu au vifaa vingine vya chuma katika mizigo yao.

Ukaguzi wa usalama unaofanywa na wakaguzi wa uwanja wa ndege huanza na kuweka mkanda, mkoba, viatu na mavazi mengine kwenye kikapu ambacho kipo sehemu ya kwanza ya ukaguzi wa usalama. Vipakatalishi pia huwekwa katika vikapu vyao. Vikapu hivyo huwekwa kwenye mkanda unaosonga na hupitia mtambo wa uyoka. Ikiwa kuna vitu vyovyote vilivyopigwa marufuku, huondolewa. Ukifika hatua hii mwonyeshe afisa hati zako za kusafiri na tikiti zako za ndege.

Baada ya hapa, karani anayehusika na usalama atamwita abiria apite mlango wa ukaguzi wa usalama. Wakati mwingine utaambiwa uvue viatu lakini afisa husika atakwambia kando. Iwapo kuna chochote ambacho si cha kawaida, afisa husika atamkagua abiria tena. Haya yote ni kwa ajili ya kuimarisha usalama wa wasafiri.

Kuabiri Ndege

Baada ya ukaguzi utaingia eneo la safari za kimataifa na uende kwenye lango ambalo ndege yako itapaa ikiwa. Utaambiwa lango wakati wa kuingia na pia limeandikwa kwenye tikiti na linaonekana kwenye mabango ndani ya uwanja wa ndege.

Utasubiri kwenye lango hadi usikie tangazo kwamba ndege iko tayari kuabiri. Wakati mwingine ndege huchelewa kuondoka na itakulazimu kusubiri kidogo. Baada ya tangazo la kwamba ndege iko tayari kuabiri, abiria wote watapanga foleni. Wakati wako ukifika mwonyeshe karani hati zako za kusafiri na tikiti yako. Baada ya kumwonyesha utapita kwenye ujia unaongia ndani ya ndege na ukae kwenye kiti kulingana na namba yako. Mabegi uliyobeba yatawekwa kwenye nafasi ya mzigo iliyo juu ya viti.

Kuna wafanyakazi kwenye ndege watakaokusaidia kipindi chote cha safari yako. Ukiwa safarini utapewa chakula na vinywaji. Kuna vyoo kwenye ndege. Wakati wa kupaa na kutua kila abiria akae kwenye kiti chake na afunge mkanda. Ni marufuku kuvuta sigara kwenye ndege na simu lazima zizimwe.

Safari ya ndege itachukua saa nyingi. Mara nyingi ndege hutua katika nchi nyingine ili kufaulisha abiria safarini. Kufaulisha kuna maana itakubidi ushuke na uingie kwenye ndege nyingine kabla ya kufika Ufini. Katika eneo la kufaulisha utaonyesha hati zako za kusafiri na tikiti zako ili uendelee na safari na unaweza kupitia ukaguzi wa usalama. Mzigo unaowekwa sehemu ya mizigo ya ndege utapelekwa Ufini otomatiki.

Kuwasili Ufini

Kuwasili nchini Ufini, Helsinki, kwenye uwanja wa ndege. Kwanza utaonyesha hati zako za kusafiri katika sehemu ya kukagua pasi. Utampa karani hati hizo. Pasi hukaguliwa ya mtu mmoja baada ya mwingine. Watoto wadogo wanaweza kuandamana na wazazi wao.

Mamlaka ya Ufini yatachukua maelezo yako ya kibinafsi, picha na alama za vidole unapowasili nchini Ufini au mara baada ya kusajiliwa kuwa umewasili.

Baada ya pasi kukaguliwa, kila mtu ataingia kwenye ukumbi mkubwa ambako utasubiria mzigo wako uliouacha katika ukaguzi wa mizigo katika nchi uliyotoka. Mzigo utafika kwenye ukanda tofauti kutegemea safari ya ndege. Unaweza kuangalia safari yako kwenye bango la umeme. Hakikisha mizigo yako yote imewasili. Kuna vigari katika ukumbi vya kubebea mizigo yako. Baada ya mizigo yote kuwasili fuata mstari wa kijani unaolekea sehemu ya kutoka. Hii ina maana kwamba huna bidhaa za kuwasilisha kwa mamlaka. Basi umeondoka sehemu ya kimataifa na unaweza kuanza safari yako nchini Ufini.

Pakua hapa yaliyomo katika kurasa huu katika muundo wa PDF.